Bilioni 3.3 za maendeleo zafika Makete, Mbunge aonya 'wizi kisheria'

WILAYA ya Makete imepokea fedha za maendeleo awamu ya kwanza kiasi cha Sh. billion 3.312 kutoka serikali kuu ambazo zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo wilayani humo.


Taarifa hiyo imetolewa na Mbunge wa Makete, Festo Sanga katika kikao kazi cha watendaji na wataalamu wa wilaya hiyo. 

Alisema: "Tumepokea fedha nyingi za maendeleo kutoka serikalini,haijawahi kutokea na hii ni awamu ya kwanza. Fedha hizi zinakwenda kwenye madarasa, zahanati, hospitali, ujenzi wa jengo la utawala n.k, niwaombe watumishi wenzangu, tukazisimamie fedha hizi kikamilifu na kwa uaminifu mkubwa.," alisema Sanga na kuongeza kuwa: 

"Tuache "Wizi wa Kisheria" wa kufuata taratibu zote za manunuzi huku tukiwa tumezidisha bei ya vitu kwa maksudi ya kujinufaisha. Mimi kama Mbunge sitawaacha salama watumishi wote watakao hujumu fedha hizi ambazo Mh Rais (Rais Samia Suluhu Hassan)ameona vyema zije ziwasaidie Wanamakete kwenye miradi yao ya maendeleo". alisema 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo