Mwanamuziki wa nyimbo za injili mjini Eldoret William Getumbe, amedhihirisha kuwa ni mwanamume anayempenda mke wake kwa njia ya ajabu sana.
Mwanamuziki huyo alipakia picha safi kwenye Facebook, iliyomuonyesha akimbeba mke wake mrembo, Virginia Masitha, mabegani mwake.
Picha hiyo ilimuonyesha Getumbe akiwa amechangamka na kudhihirisha kweli ni mwanamume 'romantic'.
Wakati TUKO.co.ke ilipomhoji, mwimbaji huyo alikiri huwa anambeba mke wake mara, angalau mara moja kwa mwezi na ni tabia mabayo huleta furaha kwenye ndoa. Getumbe amewahimiza wanaume kwenye ndoa na ambao wana madhumuni ya kuleta furaha na msisimko kwenye ndoa zao kuzoea kuwabeba wake zao mara kwa mara.
Kwa mujibu wa Getumbe, mambo rahisi kama hayo huwafurahisha sana wanawake. Msanii huyo alidai kuwa iwapo mwanamume atajitahidi kumbeba mabegani kewe angalau mara moja kwa mwezi, basi mwanamke huyo siku zote atakuwa mwaminifu na hatomchiti kamwe.
"Wanawake hupenda kutunzwa kwa mambo madogo, kumbeba kwenye mabega yako kutayeyusha moyo wake kwa mahaba. Mbebe mkeo mara moja kwa mwezi na hatochiti. Nimekuwa nikifanya hivyo na inafanya kazi vyema. Ana furaha na ni mwaminifu," Getumbe aliiambia TUKO.co.ke.
Chanzo: TUKO.co.ke