Naibu Spika,
Dk Tulia Ackson
amemkingia kifua
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kujibu swali kuhusu Serikali kulipa siku 10 Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka wake wa Pasaka uliotolewa
Machi 24, 2018, ambao mbali na masuala ya kiroho, ulitaja changamoto
tatu za kijamii.
Swali kuhusu KKKT iliyoandikiwa barua ya kutakiwa kufuta waraka huo
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, limeulizwa leo Alhamisi Juni 7,
2018 katika kipindi cha Maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu na
mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia.
Katika swali lake, Mbatia ametaka kujua ukweli kuhusu barua hizo
lakini baada ya kumaliza kuuliza swali hilo, Dk Tulia amesema haliwezi
kujibiwa na kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni.
“Kuna barua wamepewa KKKT na TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania ) wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresima,” amesema
Mbatia na kuitaka Serikali kueleza uamuzi huo una lengo gani.
Mara baada ya swali hilo, naibu spika huyo amesema, “mtakumbuka
mheshimiwa Kubenea (Saed-mbunge wa Ubungo-Chadema) alimuuliza
waziri Mkuu swali linalohusu dini na mheshimiwa Spika alizuia suali
hilo lisijibiwe.”
Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia alimuita mbunge mwingine kuuliza
swali huku Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi akiketi
na kuzungumza na na wabunge wengine wa vyama vya upinzani chini
kwa chini.