WANACHAMA WA chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)
wilayani Makete mkoani Njombe wamesisitizwa kuchangia michango mbalimbali ya
maendeleo katika maeneo wanayoishi wilayani hapa.
Akizungumza
na wanachama wake wa kata ya Ikuwo mwenyekiti chama hicho wilaya ya Makete Ibrahimu
Ngogo amesema kama mwenyekiti atafurahishwa kuona wanachadema wanakuwa mstari
wa mbele katika shughuli za maendeleo.
Mwenyekiti
Ngongo amesema pasipo kujali kiongozi anayeongoza eneo husika anatoka upande wa
chama gani cha siasa, wao wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kuchangia maendeleo.
Amesema
chama hicho kimejaliwa watu wachapa kazi hivyo wanatakiwa kuwa mfano katika kupigania
maendeleo ili taifa lisonge mbele.
Amesema
kiongozi yeyote atakayetangaza michango au shughuli ambazo ziko kinyume na
sheria za nchi wanachadema wasisite kuikataa na kuikemea.
Naye
mwenyekiti wa madiwani wa Chadema mkoa wa Njombe ambaye pia ni diwani wa kata
ya Matamba Mh Ephel Ng’ondya amesema wanachi na wanachama wa chama hicho kata
ya Ikuwo wahakikishe wanafanya kazi kwa kushirikiana na diwani wao ili
kufanikisha maendeleo.