VIDEO: Basi la Kimotco lilivyotumbukia Mtoni

Basi la Kampuni ya Kimotco lililokuwa likitoka Musoma,kwenda Arusha kupitia Mugumu,limepinduka katika mto unaodaiwa kuwa na viboko ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo William Mwakilema amethibitisha kupata taarifa ya tukio hilo leo Machi 16,na kusema kuwa katika ajali hiyo hakuna majeruhi wala vifo,na kuwa abiria wote wako juu ya basi.
Jitihada za kuwaokoa mmoja mmoja zinaendelea.Baada ya basi hilo kusombwa na maji abiria wote walitokea juu ya madirisha ya basi na kukaa juu yake,kwani halikuzama lote,jitihada za kuwaokoa zimefanyika ili kuwaokoa..


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo