Mume aua mke wake na kumficha kwenye Mbuyu

Benard Shumba (47)  mkazi wa Singida anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kumuua mke wake miaka nane iliyopita kisha kuuficha mwili huo kwenye mbuyu

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Deborah Magiligimba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema mtuhumiwa baada ya kukamatwa alikiri kutenda kosa hilo na kwenda kuonesha mwili wa marehemu aliokuwa ameuhifadhi ndani ya mbuyu.
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kupata mabaki ya mwili wa mwanamke huyo baadhi ya mifupa imechukuliwa kwa ajili yakupeleka kwa mkemia wa serikali na iliyobakia ndugu wamekabidhiwa kwa ajili ya mazishi.
Imeelezwa kwamba mnamo tarehe 7/10/2010 huko katika kijiji cha Yulansoni kata na tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama Mkoa wa Singida mwanamama Tabu Robert (28) , (mnyiramba)mkulima wa Yulansoni aliripotiwa kuuawa na mume wake aitwae Bernard Shumba mkulima wa Yulansoni


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo