Mchezaji wa Simba afariki dunia

Mchezaji wa Zamani wa timu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania, Arthur Mambeta amefariki dunia baada ya kuugua kwa kipindi kirefu jijini Dar es Salaam

Kutoka na taarifa hizo, Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema wamepokea ujumbe huo kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji huyo ambapo msiba wake unafanyikia Kigamboni.
"Tumepokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha mchezaji wa zamani wa kimataifa wa klabu yetu ya Simba Arthur Mambeta ambae amefariki jana hapa jijini. Mambeta anakumbukwa sana na wanasimba pale alipotoka kwenye kustaafu soka na kuja kuisaidia klabu yake kuifunga klabu ya Yanga kwenye mchezo wa fainali Ligi kuu goli 1-0. Hiyo ilikuwa mwaka 1973 huko nyuma mchezaji huyo alikuwa ni mshambuliaji mahiri kabla ya kuja kucheza beki", amesema Manara.
                                        Marehemu Arthur Mambeta  enzi za uhai wake.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo