Mawaziri wagomea mkutano wa Rais Magufuli?

Waziri wa Kilimo, Mhe. Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na Rais Dkt Magufuli

Katika mkutano huo Rais Magufuli aliwahitaji mawaziri hao ili waweze kutoa ufafanuzi kuhusu maswala ambayo yameibuliwa na wafanyabiashara katika mkutano huo lakini ikaonekana mawaziri hao pamoja na Makatibu wao hawajafika licha ya kuwa walialikwa na kupaswa kuwepo kwenye mkutano huo. 
Kufuatia kutokuwepo Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri Mkuu alipojibu kuwa walipata mwaliko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote wao kutokuwepo wala kutuma wawakilishi wao. 
"Kwa hiyo wa Kilimo na Mifugo mawaziri na Makatibu wakuu wote hawapo? Wao sio wajumbe wa mkutano huu? Alihoji Rais Magufuli ndipo Mawaziri Mkuu aliibuka na kutoa majibu kwa Rais Magufuli. 
"Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na kusupport uchumi wetu wa viwanda, kilimo ni facilitater wa viwanda na Mifugo naye pia ni wa viwanda walikuwa wapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa taarifa wote" 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo