MKUU
wa shule ya sekondari Lupalilo iliyopo wilayani Makete mkoani Njombe Johnes
Liombo amekishukuru kituo cha Green fm Redio na
wadau wengine walioshiriki katika
kuhakikisha umeme unarejea katika shule hiyo.
Mwalimu
Liombo amezitoa Shukrani hizo February 12 shuleni hapo wakati akizungumza na blog hii,
katika
shukrani hizo amesema Tanesco, mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya Makate mh,Egnatio Mtawa na uongozi mzima wa wilaya
umeshiriki kwa kiwango kikubwa katika kuhakikisha umeme unarejea shuleni hapo.
Ameongeza
kuwa katika shule hiyo tangu ilipoharibika Transfoma zaidi ya mwezi mmoja
uliopita wanafunzi walipata changamoto kubwa katika kujisomea wakati wa usiku.
Amesema baada ya kupeleka
taarifa Tanesco aliambiwa transfoma
inapoharibika taratibu maalumu zinafanyika kuhakikisha nyingine inapatikana.
Baada
ya jitihada zao Tanesco wemefunga transfoma nyingine ya muda shuleni hapo ambayo ipo kwa kipindi ambacho shirika hilo
la umeme linaendelea na jitihada za kuhakikisha transfoma yenye uwezo kama ile
ya awali iliyoungua ianapatikana.
Pamoja
na hayo amesema transfoma hiyo inafanya kazi vizuri kwa kiasi kikubwa na
kuepusha adha ya kushindwa kusoma kwa wanafunzi
licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo muda Fulani huwa umeme na kukata
ambapo yeye kama mwalimu amesema hajaona kama tatizo kubwa.
Kwa
upande wao wanafunzi wasichana Ruth John na Clara James ambao ndio wanaokaa
shuleni wamesema wamefurahishwa na
kitendo cha umeme kurejea shuleni hapo ambapo kwa sasa wanauwezo wa kijisomea
muda wowote hasa nyakati za usiku,pia wanaimani kubwa na usalama wao wakiwa
shuleni.