"Tundu Lissu asingepona" - Mwigulu Nchemba

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amefunguka na kuweka wazi kuwa baadhi ya wanasiasa wanaohubiri sakata la Lissu kupigwa risasi wanafanya siasa kwani ukweli ni kwamba bila serikali kiongozi huyo angekuwa amepoteza maisha

Mwigulu amesema hayo leo Februari 14, 2018 akiwa Singida na kudai kuwa bila jitihada za serikali huenda Mbunge huyo wa Singida Mashariki Tundu Lissu angekuwa amepoteza maisha kufuatia shambulio la kupigwa risasi akiwa mjini Dodoma. 
"Lissu aliposhambuliwa daktari aliyekwenda kuokoa maisha yake yaani huduma ya kwanza ile ambayo isingefanyika Lissu angepoteza maisha yake ilifanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ambaye ni mteule wa Rais, Katibu Mkuu alikwenda kuvaa joho kwa sababu yeye ndiye mtalaam aliyebobea ili aokoe maisha ya ndugu yetu, basi daktari yule pamoja na madaktri wengine ambao wao ndiyo Serikali wasingefanya huduma ya kwanza ile ya kuzuia damu kutoka ndugu yetu asingepona" alisisitiza Mwigulu Nchemba 
Mwigulu aliendelea kuzungumza 
"Hawa wanakuja wanaongea ongea juu ya Lissu hata hawatokei hapa Singida angekuwa mtu anayetokea Singida ilibidi aipongeze Serikali kwa kazi iliyofanya baada ya Lissu kushambuliwa" alisisitiza 
Mbali na hilo Mwigulu Nchemba amewataka wanasiasa kutotumia tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi na kufanyia siasa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo