News Alert: Orodha ya Watumishi wa Umma wanaostahili Kulipwa Madai Yao

Wizara ya Fedha na Mipango Inapenda kuwajulisha Watumishi wa Umma kuwa, kikosi kazi kimemaliza uhakiki wa madai ya malimbikizo ya mishahara, zoezi hilo lilikamilika tarehe 5 Februari, 2018. Baada ya zoezi la uhakiki wa Watumishi wa Umma kukamilika, Serikali imejipanga kuanza kulipa madai sahihi kupitia kwenye Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS) kwa mkupuo mwezi Februari, 2018.
Aidha, Wizara ya Fedha na Mipango inawatangazia Watumishi wa Umma waliokuwa na madai hayo kuwa orodha ya majina ya wanaostahili kulipwa kutokana na Uhakiki huo kukamilika yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango ambayo ni www.mof.go.tz na Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo www.maelezo.go.tz
Imetolewa na;
KATIBU MKUU – WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
10 Februari, 2018


Kupata Majina ya Watumishi wa Umma wanaostahili Kulipwa Madai ya Malimbikizo ya Mishahara,

BONYEZA HAPA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo