Akizungumza kwenye mkutano wa jopo la viongozi mbalimbali duniani lililoundwa kuangalia mfumo wa kuhudumia wakimbizi na jinsi ya kumaliza migogoro iliyopo katika nchi mbalimbali, jijini Dare s Salaam, Dk. Kikwete amesema, jopo hilo pamoja na mambo mengine limekutana kupokea taarifa ya changamoto na kujua jinsi gani nchi zenye uwezo mdogo zinaweza kusaidiwa na Jumuiya ya Kimataifa.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dk. Augustine Mahiga, amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kutoendelea kuwapa nafasi ya ajira, umiliki wa ardhi na ukazi wa kudumu wakimbizi kwa kutumia mkopo wa Benki ya Duniani bila kuzingatia mikataba ya Kimataifa iliyopo na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa ingilie kati suala hilo.
Aidha amesema, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kujiridhisha na kuona ukiukwaji wa mikataba ya kimataifa ya kusaidia wakimbizi inakiukwa pamoja na msaada wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi, UNHCR bado halikidhi mahitaji yaliyopo na kukanusha si kweli kwamba Tanzania haitaki kusaidia wakimbizi.