Mapacha waliozaliwa Rukwa wapewa majina ya Lissu, Mbowe na Halima Mdee

MAPACHA WATATU WAPEWA MAJINA HALIMA MDEE, MBOWE NA LISSU
*Ni Sumbawanga mkoani Rukwa
*Uchungu ulimshika baada ya kusikia ujio wa Halima Mdee

Mwanamke mmoja Martha Alphonce Haule mkazi wa Kata ya Nafulala, Sumbawanga mkoani Rukwa amejifungua watoto mapacha watatu na kuwapatia majina ya Halima Mdee (wa kike) pamoja na Mbowe na Lissu (wakiume wawili).

Watoto hao ambao wana mwezi mmoja wamezaliwa kufuatia mwanamke huyo kupata uchungu ghafla baada ya kusikia Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa Mhe. Mdee atazuru Sumbawanga na kutembelea kikundi chao cha Wanawake Tunaweza kilichopo katika Kata ya Mafulala.

Mwenyekiti huyo wa BAWACHA leo tarehe 11 januari 2018 akiwa katika siku ya pili ya ziara yake yenye lengo la ujenzi na uenezi wa chama ikiwa ni pamoja na kuangalia uhai wa baraza hilo na kutoa mwongozo wa shughuli mbalimbali za kichama ametembelea kikundi hicho cha kina Mama na kuwaona watoto hao na pia kama Baraza wamechangia kikundi hicho shilingi 200,000 ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi za wanawake hao.

Awali katika ziara hiyo ambayo ameongozana na Katibu wa BAWACHA Taifa Mhe. Grace Tendega, Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA Mhe. Suzani Mgonukulima, Mbunge Viti Maalumu Mhe. 

Aida Khenan na Viongozi BAWACHA Rukwa walitembelea vikundi vingine vya wanawake vya Sayari, Tupendane (Katandala) na kuweza kuongea nao pamoja na kuchangia fedha kama ishara ya kuunga mkono juhudi za wanawake hao.

Habari - CHADEMA
Kanda ya Nyasa
10 Januari, 2018
Image may contain: 4 people, people smilingImage may contain: 1 person, smiling, standingImage may contain: 5 people, people smiling, people standingImage may contain: 10 people, people standing, crowd, sky and outdoorImage may contain: 17 people, people smilingImage may contain: 2 people, people smiling, people standing and outdoorImage may contain: 13 people, people smiling, stripes and outdoorImage may contain: 1 person


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo