BREAKING: Lowassa Akutana na Freeman Mbowe Kumpa Mrejesho wa Ikulu

Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amekutana na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho wa alichozungumza na Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na waraka na taarifa nyingi za kupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.

“Taarifa zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh Lowassa. Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na mwenyekiti wa chama chake, Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.”

“Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki , taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala wao,”

“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”
============================



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo