Wanaonunua 'machangudoa', kushughulikiwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro, amesema wanafikiria kuanza kuwakamata wanaume ambao wananunua wadada wanaojiuza (Machangudoa) katika mitaa mbalimbali ya Kinondoni

Kamanda Muliro ameyasema hayo leo kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio ambaspo amesisitiza kuwa, kufanya hivyo itasaidia kupunguza wateja na hivyo wadada hawatajiuza tena kwasababu watakosa wateja.
“Nafikiri kama wanaume wangekubali kutokwenda kwa hao madada poa hiyo biashara ingekufa sasa nafikiri badala ya kuwakamata tu hao wadada, wasishangae kwa mkoa wa Kinondoni tukaanza kuwakamata hao wanaume na kuwafikisha mbele ya sheria”, amesema Kamanda Muliro.
Aidha Kamanda Muliro amesema Jeshi la polisi Kinondoni limejipanga kuhakikisha wananchi wakiwemo wafanyabiashara wanafanya shughuli zao kwa amani na usalama kwenye sikukuu ya mwaka mpya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo