Polisi wafunguka juu ya kukamatwa Askofu Kakobe

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi mpaka sasa halijamkamata Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zakaria Kakobe kama baadhi ya taarifa zinavyosamabazwa

Kamanda Mambosasa amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa bado hawajamtia nguvuni Askofu huyo na pindi watakapomkamata kwa makosa aliyotenda basi watatoa taarifa hizo. 
"Baba Askofu Kakobe bado hatujamkamata pale atakapokuwa amekamatwa kwa makosa aliyotenda nitawaambia lakini kwa sasa hajakamatwa mchungaji huyo, jeshi la polisi huwa halipangi kumkamata mtu bali mtu anapofanya kosa la jinai ndipo anakamatwa hivyo na yeye kama amefanya kosa hili basi tutamkamata" alisisitiza Mambosasa 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo