News Alert: Rais Magufuli amteua mtu wa kuchunguza mali za CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli ameunda tume ya watu tisa  kufuatilia mali za chama hicho, akiifananisha na tume aliyoiunda kuchunguza biashara ya madini nchini.
Miongoni mwa wajumbe wa tume hiyo itakayoongozwa na Dk Bashiru Ali Kakurwa, ni kada mpya wa chama hicho, Albert Msando aliyejiunga na CCM Novemba 21 akitokea ACT-Wazalendo.
Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Jumatano Desemba 20,2017 mjini Dodoma katika kikao cha kwanza cha Halmashauri Kuu (NEC) ya chama hicho kilichojadili mikakati ya kuimarisha kazi za CCM na Serikali.
Wajumbe wengine wa tume hiyo ni Walter Msigwa, Galala Wabanhu, Albert Chalamila, William Sarakikya, Komanya Kitwara, Dk Fenela Mukangara na Mariam Mangula.
"Nataka nitoe wito na Waziri Mkuu yuko hapa, hii timu itachunguza mtu yeyote awe wa Serikali au kwenye chama ili mali zote ziorodheshwe," amesema katika taarifa zilizotolewa na chama hicho.
"Hii ni tume yangu, ni kama ya makinikia ila haya ni makinikia ndani ya CCM. Nataka siku moja chama hiki kiweze kujitegemea," amesema.
Mwenyekiti huyo wa CCM amewataka Watanzania wanaoshikilia mali za chama hicho kujitokeza na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa masilahi ya CCM.
CCM
MAGUFULI AMTEUA DKT BASHIRU ALI KUCHUNGUZA MALI ZA CCM- Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais John Pombe Magufuli ameunda tume ya chama itakayokuwa na jukumu la kwenda kufuatilia mali za CCM kote nchini. Kamati hiyo itakuwa chini ya mwenyekiti Dkt Bashiru Ali Kakurwa ambae atasaidiwa na wajumbe nane ambao ni Walter Msigwa, Albert Msando, Galala Wabanhu (Hananasif), Albert Chalamila, William Sarakikya, Komanya Kitwara, Dkt Fenela Mkangara na Mariam Mungula.
Posted by Azam TV on Wednesday, December 20, 2017


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo