Nape Nnauye ahoji upatikanaji Mwenyekiti wa Chama

Mbunge Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni kwa kuhoji vyama vya siasa na wanasiasa Tanzania wanajifunza nini kufuatia mchakato wa uchaguzi ndani ya chama tawala cha (ANC) uliofanyika Afrika Kusini mwanzoni mwa wiki hii kumpata kiongozi wa chama hicho

Chama tawala cha African National Congress (ANC) kilikuwa na uchaguzi wa ndani kumtafuta kiongozi wa juu ya chama hicho ambapo kulikuwa na zoezi la uchaguzi na nafasi hiyo kugombewa na wananchama wa chama hicho na kupigiwa kura, ambapo mwisho wa siku Cyril Ramaphosa aliibuka mshindi kwa kura nyingi zaidi dhidi ya Nkosazana Dlamini-Zuma hivyo Cyril Ramaphosa kutangazwa Rais wa (ANC). 
"Tunajifunza nini kwa mchakato uliopelekea kupatikana kwa Cryll Ramaphosa kama Mwenyekiti wa ANC!? Alihoji Nape Nnauye 
Uchaguzi wa Chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) ulitoa nafasi ya watu kugombea nafasi hiyo na kuleta ushindani ambapo wanachama wa chama hicho walipiga kura na kuweza kumpta mshindi ambaye ndiye alitangazwa kuwa kiongozi mku wa chama hicho


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo