Lissu: "Walikuwa watu wawili, mmoja mwembamba niliona akishuka huku ameshika "Machine gun"

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kupitia CHADEMA amesema anaendelea vizuri  na atarejea nchini akiwa salama

Lissu ameyasema hayo leo mchana wakati akifanya mahojiano na idhaa ya Kiswahili ya Kijerumani (DW).
"Madaktari wangu wamenihakikishia kuwa nitarejea nchini na nitaendelea na shughuli zangu kama kawaida", amesema
Katika hatua nyingine Lissu amesema anachokumbuka katika tukio hilo wakati wanaingia getini kulikuwa na gari moja nyeupe limesimama huku kulikuwa na watu wawili.
"Walikuwa watu wawili, mmoja mwembamba niliona akishuka huku ameshika "Machine gun" baadaye najishtukia nipo hospitali Nairobi", ameongeza.
"Ninachoshangaa ndani ya ile nyumba kuna ulinzi mkali walikuwa wapi walinzi wakati nashambuliwa", amesema.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo