Lissu: Nimeambiwa na Daktari nitasimama tena

Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu amefunguka na kusema kuwa ameambiwa na madaktari wake kuwa atasimama, atatembea na kurudi tena Tanzania kuendelea na majukumu yake kama kawaida

Tundu Lissu amesema hayo leo alipofanya mahojiano na DW na kusema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri kiafya na kuwa madaktari wamemweleza kuwa atasimama na kutembea tena kama zamani na kurudi nyumbani kwake Tanzania.
Aidha Tundu Lissu amesema hajapoteza matumaini ya kuwapata na kuwatambua watu ambao walishambulia kwa risasi kwa kuwa anaamini sehemu ambayo tukio hilo lilitokea kulikuwa na ulinzi na walinzi wa serikali.
"Matumaini hayajapotea kwa vile nakaa kwenye nyumba za serikali hizi nyumba zinalindwa masaa 24, Je, siku hizo napigwa risasi walinzi walikuwa wapi? Walinzi wa geti kubwa nao walikuwa wapi? Ile sehemu yote tunayoishi imezungushwa ukuta na kuna geti kuu lenye ulinzi masaa 24 nao walikuwa wapi? alihoji Tundu Lissu 
Mbali na hilo Tundu Lissu ameelezea jinsi ambavyo tukio hilo lilitokea mnamo Septemba 7, 2017 pale Dodoma msikilize hapa chini akitolea maelezo hilo. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo