TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa orodha ya wanachama 15 wa vyama vya siasa walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido.
Tume pia imetoa orodha ya majina ya wanachama wengine 15 wa vyama mbalimbali ambao wamejitokeza kugombea udiwani katika uchaguzi mdogo unaofanyika kwenye kata sita.
Walioteuliwa kugombea ubunge katika jimbo la Longido ni Kisiongo Mayasek Olokuya (CUF), Francis Ringo (CCK), Dk Steven KIruswa (CCM), Mgina Mustafa (AFP), Godwin Sarakikya (ADA TADEA), Feruziy Furuziyson (NRA), Ngilisho Paul (Demokrasia Makini), Simon Bayo (SAU) na Robert Lukumy (TLP).
Waliojitokeza kugombea ubunge katika jimbo la Singida Kaskazini ni Omari Sombi (AFP), Dalphina Mlelwa (CUF), Monko Joseph (CCM),David Djumbe (Chadema), Aloyce Nduguta (ADA TADEA) na Mchungaji Yohana Labisu (CCK)
Katika uteuzi huo pia kuna walioteuliwa kugombea udiwani katika kata ya Kimandolu ambako kuna wanachama wa vyama vitano vya Gaudence Lyimo (CCM), |Rashid Nyawaya (CUF), Hamis Mgoya ( NRA), RAmadhani Mcharo (Demokrasia Makini), na Shafii Kiktunda (SAU).
Katika kata ya KIhesa halmashauri ya Iringa Mjini ameteuliwa Sawani Juli (CCM), Kata ya Keza wilayani Ngara walioteuliwa ni Eradiu8s Bitemele (NCCR Mageuzi), Bakundukize Gwaibondo (CCM), Philipo Bazubwenge (CUF). Kata ya Kurui wilayani Kisarawe wagombea ni Kunikuni Salumu (CCM) na Kikumbi Mwalimu (CUF),
Kata ya Bukumbi wilaya ya Uyui wagombea ni Kasoga Sizya (CCM), Edward Msigala wa (CUF) wakati kata ya Kwagunda wilaya ya Korogwe walioteuliwa ni Said Shenkawa (CCM) na Yusuf Senkawa wa CUF.