Lazaro Nyalandu amuandikia Rais Magufuli ujumbe

Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Singida Kaskazini leo Disemba 11, 2017 ametuma salamu za pole kwa Rais John Pombe Magufuli kufuatia vifo vya askari 14 wa JWTZ waliouawa nchini DRC Congo na miili yao kusafirishwa na kuwasili leo Tanzania

Nyalandu ametumia ukurasa wake wa Facebook kutuma salamu zake za pole kwa Rais Magufuli na familia mbalimbali za askari hao waliouwawa na wale waliojeruhiwa katika mapigano makali yaliyotokea nchini DRC Congo Disemba 7 na 8 kati ya askari wa Tanzania na Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) yaliyopelekea askari hao 14 wa Tanzania kupoteza maisha huku wengine 44 wakiwa wamejeruhiwa na wawili wengine mpaka sasa hawajulikani walipo. 
"Natoa pole kwa Mhe. Rais Magufuli na wanafamilia wote kufuatia kuuawa kwa maaskari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)" alindika Nyalandu  
Miili ya wanajeshi 14 wa JWTZ ambao wameuawa nchini DRC Congo imewasili leo jijini Dar es Salaam kwa ndege maalum ya Umoja wa Mataifa, baada ya hapo miili hiyo itapelekwa kwenye hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo