IGP Sirro amesema hayo leo Disemba 21, 2017 akiwa mkoani Lindi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa tuhuma zinazotolewa na viongozi wa upinzani kuhusu baadhi ya polisi kuwatoa wasimamizi wa uchaguzi si za kweli kwa kuwa mpaka sasa hajapokea barua au malalamiko ndani ya ofisi yake kutoka kwa viongozi hao wa upinzani nchini.
Mbali na hilo IGP Sirro amedai kuwa jeshi la polisi nchini limejipanga vyema kuimalisha ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka
Aidha IGP Sirro mara baada ya kufika mkoani Lindi aliweza kukutana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na pia akatembelea kambi ya kisosi ya kutuliza ghasia
aliweza kuangalia mazoezi mbalimbali yanayofanya na jeshi la polisi mkoani Lindi.
aliweza kuangalia mazoezi mbalimbali yanayofanya na jeshi la polisi mkoani Lindi.