Heche: "CCM kama mnataka kujibu hoja za Askofu Kakobe kwa niaba ya Rais Magufuli na Serikali jibuni kwa hoja, sio kuropoka!

Mbunge wa wa Tarime John Heche amewaonya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kuwa kama wanataka kumjibu Askofu Zacharia Kakobe kwa niaba ya serikali iliyopo madarakani basi wajibu  kwa hoja na siyo kuropoka

Heche amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kamugisha kumtaka Askofu Kakobe aende kufanya toba na kisha kuwaomba radhi wana CCM wa Dar es salaam kwa kuacha miiko ya kidini na kushindwa kutumia busara na kisha kusema hovyo.
Akizungumza jana na Wanahabari Kamugisha alivitaka vyombo vinavyohusika na sheria vihakikishe hakuna mtu anayepata fursa ya kumtukana au kumbeza Rais wa nchi na kufafanua kwamba Rais amejipambanua katika kuwasaidia wananchi na anafanya mambo hayo kwa udhati wa moyo wake hivyo mtu anyebeza moja kwa moja atakuwa msaliti.
Heche amandika kwenye ukurasa wake wa Twitter na kusema kwamba "CCM kama mnataka kujibu hoja za Askofu Kakobe kwa niaba ya Rais Magufuli na Serikali jibuni kwa hoja, sio kuropoka! kazi za wachungaji ni kukemea maovu yote yaliyopo duniani, watu wanapotea, wanapigwa risasi, wanaokotwa baharini, sheria za nchi hazifuatwi, haya yatakemewa na kila mtanzania" Heche.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo