Moto wateketeza nyumba Ubungo

Moto mkubwa ambao chanzo chake bado hakijajulikana umeteketeza nyumba moja katika eneo la Ubungo kwa Mbonde asubuhi hii




Wananchi wa eneo hilo waliendelea na jitihada za kuzima moto huo, lakini kutokana na kuwa mkubwa zaidi jitihada hizo zilishindikana.
Tayari kikosi cha jeshi la zimamoto kimewasili eneo la tukio ili kuzima moto huo pamoja na mafundi wa umeme kutoka Tanesco kitengo cha dharula ili kukata umeme kuzuia madhara zaidi.
Bado hakujatolewa taarifa yoyote ya vifo au majeruhi, 
Endelea kubaki nasi 
Kikosi cha zimamoto kikiwasili eneo la tukio
Tanesco wakiwa wamewasili eneo la tukio
Nyumba ambayo inateketea kwa moto. Chanzo: EATV


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo