Kwenye ukurasa wake wa Facebook Zitto Kabwe amesema amekuwa na utaratibu wa kutembelea wavuti ya BOT na kukuta machapisho ya hali ya uchumi tangu akiwa chuo kikuu, lakini kuanzia mwezi Juni 2017 mpaka mpaka sasa BOT haijaweka taarifa hizo wazi.
“Tangu nianze kusoma taarifa hizi nikiwa chuo kikuu hii ni mara ya kwanza imepita miezi 4 MER haijachapishwa kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania. Mara ya mwisho imewekwa taarifa ya mwezi June inayoeleza mapitio ya mwezi Mei 2017. Taarifa hiyo ya mwisho ilionyesha kuwa mauzo yetu nje kwa bidhaa za viwanda yameporomoka kwa zaidi ya USD 700 milioni sawa na Bombadier mpya 21 Hivi”, ameandika Zitto Kabwe.
Zitto Kabwe ameendelea kwa kusema kwamba kitendo hicho kinawanyima wananchi uhuru wa kujua hali ya uchumi, na ana wasi wasi wasi kuwa taarifa ambayo itakuja kutolewa itakuwa ya kupikwa pikwa.
Mnamo tarehe 27 Agosti 2017, Mbunge Zitto Kabwe aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa facebook akisema uchumi wa nchi unazidi kushuka, licha ya kuwepo kwa takwimu kwamba uchumi unapanda hadi kufikia nchi ya pili Afrika miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unatazamiwa kwa kasi.
Alichokiandika Zitto Kabwe facebook
