Waziri Mwakyembe avionya vyombo vya habari

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema Serikali inatambua haki ya vyombo vya habari katika kukosoa, kujadili na kuchambua masuala mbalimbali na kuviasa visivuke mipaka na kuhatarisha masilahi ya Taifa katika kufanya kazi zake.

Dk Mwakyembe amesema hayo leo Jumatano Oktoba 25,2017 katika mkutano na viongozi wa madhehebu ya dini uliojadili masuala ya amani na uzalendo kuelekea uchumi wa viwanda.
Dk Mwakyembe amesema Serikali inatambua uhuru wa vyombo vya habari lakini amewataka wamiliki wake na waandishi kwa jumla kufahamu sheria na vifungu vya Katiba ili kulinda masilahi ya Taifa katika utoaji wa taarifa.
Waziri Mwakyembe amesema katika kufikia uchumi wa viwanda vyombo vya habari ni vya muhimu ili kufikisha taarifa. Amewataka waandishi wa habari kuzingatia weledi ili Taifa liendelee katika sekta mbalimbali na kufikia uchumi wa kati.
Aidha Mh. Mwakyembe ameongeza kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari vinavyofuata sheria na weledi wa utangazaji ili kuimarisha amani na mshikamano kwa wananchi na kuepuka migogoro.
Naye Mchungaji Dk. Vernon Fernandes na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salimu kwa pamoja wameitaka jamii kuzingatia na kudumisha misingi ya amani kwa kuzingatia maadili ya dini, huku wakiwasihii wasomi na viongozi ni wakati wao wa kukemea mambo maovu ikiwemo rushwa na ufisadi.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo