Waliokufa kwa Mafuriko Dar waongezeka

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wamekufa kufuatia mvua kubwa zilizonyesha jana Alhamisi maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar.

Mambosasa ameyasema hayo leo Ijumaa wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Polisi Kanda Maalum.

“Ikumbukwe kwamba usiku wa kuamkia jana, mvua kubwa ilinyesha na kusababisha mafuriko ambayo yameleta maafa ndani ya jiji letu, marufiko ambayo hayajatokea siku za hivi karibuni.

“Maeneo ya Tabata uliokotwa mwili mmoja wa kijana ambaye alisombwa na maji hayo, eneo la Mbezi Luis, gari lilitumbukia mtaroni ambako pia kifo kimoja kimeripotiwa kutokea, na mtoto mdogo amethibitika kufariki kutokana na mvua hizo.” alisema Mambosasa.

Aidha Mambosasa amesema madhara ya mali zilizoharibika bado jeshi hilo halijapata thamani yake huku akieleza kuwa hakuna majeruhi aliyeripotiwa kutokana na tukio hilo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo