Wito umetolewa kwa
Wahitimu wa mafunzo ya ualimu mwaka wapili na watatu katika chuo cha ualimu
Tandala kuwa mfano mwema katika jamii
kwa kufanya matendo mema pindi wanapohitimu chuoni hapo
Wito huo umetolewa na
mgeni rasmi Afisa elimu sekondari wilaya ya Makete Jackobo Meena katika
mahafali ya 41 kwa walimu wa awali na
msingi ambapo amesema wahitimu hao
wanatakiwa kufanya mambo mazuri katika jamii na kutojiingiza kuwa watenda maovu
huku akiwakumbusha kuwa mwalimu ni kioo cha jamii
Awali wakisoma Risala
kwa mgeni rasmi wahitimu hao wamezitaja changamoto mbalimbali zinazowakabili
kama uhaba wa vyumba vya madarasa, maktaba viwanja vya michezo, kukosa
zahanati, usafiri pamoja na chumba cha
ITC
Akimkaribisha mgeni
rasmi, makamu mkuu wa chuo hicho amewapongeza wahitimu na kuwatakia maisha mema
huku akiwasisitizia nidhamu na maadili kwa pamoja na uwajibikaji
mahafali hayo ni
ya 41
ambapo wahitimu 186 wamehitimu
katika ualimu msingi yaani ordnary diploma in primary education na ualimu awali
yaani odinary in Early childhood care and education
Na Riziki Manfred