Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa kukabidhi kivuko hicho kwa chama cha walemavu mkoa wa Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikata upete wa kuashiria kivuko kimezinduliwa rasmi
Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na mmoja wa walemavu akipita katika kivuko hicho
Mmoja wa watu wenye ulemavu akipita kwenye kivuko hicho kuelekea kwenye ofisi zao za chama cha walemavu mkoani Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa viti maalum mkoani
Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amewajengea kivuko
walemavu katika ofisi yao kwa lengo la kuwarahisishia kufika ofisni hapo.
Akizungumza wakati wa
kuzindua kivuko hicho Mb Kabati alisema kuwa lengo la kuwasaidia mara kwa mara
watu wenye ulemavu ni kutokana kuwa kila mtu ni mlemavu mtarajiwa.
“Unajua hakuna mtu aijua
kesho yake hivyo usipowajali walemavu leo hata wewe kesho ukiwa mlemavu watu
hawata wajali mimi binafsi nawajali sana walemavu kwa kuwa nao ni binadamu kama
binadamu wengine” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa ametumia
gharama zake binafsi kujenga kivuko hicho ambacho kitakuwa msaada kwa watu wote
wenye ulemavu kufika ofisini kwa urahisi kabisa tofauti na ilivyokuwa hapo
awali.
“Saizi naona mambo yatakuwa
safi maana kila kitu naona kimetuwa bora na mafundi wamejenga vizuri na kivuko
hiki naona ni imara sananaombeni na nyinyi mkitunze sana hiki kivuko” alisema
Kabati
Kwa upande wake makamu
mwenyekiti wa chama cha walemavu mkoa wa Iringa (CHAWATA) Rukia Makweta alimshukuru
mbunge huyo kwa kuwajengea kivuko hicho maana kimewaondolea adhabu ya kudondoka
dondoka wakati wanaingia ofisini kutokana na ubovu uliokuwepo
.
“Unajua hiki kivuko kilikuwa
na mashimo mengi hivyo ilikuwa kazi kubwa kufika ofisini maana walemavu wengi
walikuwa wanaanguka sana katika eneo hili hivyo kujengwa kwa kivuko hiki
walemavu wengi watakuwa wanakuja ofisini bila woga wa kuanguka” alisema Makweta