Mama huyo siku ya leo alionekana Mahakama Kuu jijini Dar es salaam akiangalia mwenendo wa kesi hiyo huku akionekana kukosa furaha kabisa.
Muigizaji Bond Bin Sinnan ameandika ujumbe kuonyesha kusikitishwa na jinsi mama huyo anavyoteseka na maisha.
“Siku zote huwa nikikutizama naishiwa nguvu mwilini na amani moyoni mwangu. Huwa najiuliza mengi sana. Nikimtizama Diamond anavyo mlea mama yake nakumbuka Steve alivyokuwa anakulea wewe. Nikuombee kwa Mungu azidi kukupa nguvu na ujasiri na uamini binaadamu hajiendeshi bali huendeshwa na mungu,” aliandika Bond.
Kesi ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael inayomkabili ya kumuuwa muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia imeendelea tena Alhamisi hii katika Mahakama Kuu ambapo wazee wa baraza watatoa mtazamo wao wa mwenendo wa kesi hiyo kabla ya kuhumu.