"Wenye Ikulu ni nyinyi" - Magufuli

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa, Dkt. John Magufuli amewapongeza wajumbe waliohudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM huku akiwataka watembee kifua mbele kwa kuwa Ikulu ni yao kwa maana bila ya wao yeye asingekuwepo hapo

Dkt. Magufuli amesema hayo wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyikia katika kumbi za mikutano ndani ya Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Septemba 30, 2017 na kuendelea hadi Oktoba mosi mwaka huu.
"Kikao nimekifungua rasmi kuanzia muda huu, na niwathibitishie ndugu wajumbe kuwa Chama cha Mapinduzi ndiyo chama, hata vyama vingine vinayategemea matokeo mtakayofanya leo. Hiki chama ni imara kilicho asisiwa tangu za enzi ya Baba wa Taifa na tutaendelea kulisimamia taifa kwa manufaa ya taifa hili", amesema Dkt. Magufuli
Pamoja na hayo Dkt. Magufuli ameendelea kwa kusema "Napenda kuwa karibisha kwa mara nyingine tena hapa Ikulu. Ikulu ni kwenu, wenye Ikulu ni nyinyi, tembeeni kifua mbele kwa sababu nyinyi ndiyo mliyonichagua mimi. Msingenichagua nisingeweza kufika Ikulu kwa hiyo mjione mpo katika nyumba yenu kama ilivyo nyumba ya watanzania wote", amesema Dkt. Magufuli.
Mtazame hapa chini Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Taifa, Dkt. John Magufuli akiendelea kuchanganua baadhi ya mambo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo