FULL AUDIO: CCM yafutilia Mbali Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Makete

Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC), umefuta uchaguzi wa wenyeviti katika wilaya nne baada ya kubaini wagombea waliojitokeza hawakua na sifa.

Akitangaza uamuzi huo leo , Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, amezitaja wilaya hizo zilizofutiwa uchaguzi kwamba ni Moshi Mjini, Siha, Hai, pamoja na Makete.

Amesema sababu ya kufuta matokeo hayo ni kubainika kwamba wagombea waliojitokea hawakuwa na sifa, pamoja na kubainika kuwepo na viashiria hatarishi kwa chama.

Hivyo kutokana na uamuzi huo Polepole amesema kwamba wilaya hizo zitaanza upya mchakato wa uchaguzi huo.

Msikilize mwanzo mwisho kwa kubonyeza Play hapo chini:-


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo