Zitto Aeleza Kwa Nini Hakamatwi na Polisi Licha ya Kuikosoa Serikali

Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa ni mwanasiasa na upinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali, atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi.

Akiwajibu wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho.

“Sitaki na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria mpaka ndoto zao zilipotimia.

“Kagame alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa, Meles mpiganaji dhidi ya The Derg akiwa na umri mdogo wa miaka 19 mpaka 36 akawa Rais wa Ethiopia 39 hakukamatwa”, aliandika Zitto Kabwe.

Hivi karibuni mwanasiasa na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alikamatwa na polisi kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uchochezi.



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo