Rais Magufuli amezungumza hayo alipokuwa akizindua mradi wa maji Sengerema, na kudai kuwa wapo viongozi waliokuwa tayari kuuza maisha ya watanzania hata kwa kupewa gari ndogo tu.
"Mtu alikuwa yuko radhi kuuza maisha ya watanzania kwa Pick-Up, anaachia kila kitu, yaani tumefanya mikataba ya hovyo. Tanzania tumebinafsisha viwanda vyetu vingi, siwalaumu viongozi waliofanya hivyo ila sizuiliwi kuongea ukweli huu, yaani tulibaki kuuzwa sisi. Kuna viwanda vingine vipo Morogoro pale watu wanafugia mbuzi", alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli ameutaka uongozi wa Mwanza kufanya uchunguzi juu ya upotevu wa fedha zaidi ya bilioni mbili za maji, na kuwataka watu waliohusika kuiba fedha hizo waanze kuzirudisha wenyewe kabla ya uchunguzi huo kufanyika.
Rais Magufuli yupo ziarani kikazi jijini Mwanza kwa siku mbili