Ameyasema hayo leo (alhamisi) wakati akizungumza wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya siku tatu, mkoani Pwani.
“Nimechoka kuwalisha wafungwa, mtu afungwe halafu anunuliwe chakula. Nimeshatoa maagizo, wafungwa hawa wakalime ili waogope kufungwa,” amesema na kuongeza;
“Wakajifunze kulima, wajue kufungwa ni kufungwa na neno kufungwa ni kufungwa kweli. Tukianza kuwapunguzia maeneo magereza, mnataka wakalime wapi?” amehoji.
Rais amesema, hiyo ndiyo sababu ya kutunza maeneo ya magereza ili yatumike kwa uzalishaji mali.
Ameongeza kuwa ni vizuri wahalifu wakatumia nguvu kama walizotumia kuiba, ili wakalime.
“Huko magereza wafanye kazi, bila kujali vyeo walivyokuwa navyo, umaarufu wao na wakafanye kazi,” amesema