Jamaa abebeshwa Maiti ya Mwanaye Makambako Njombe


NJOMBE.
Mtu mmoja ambaye amefahamika kwa jina la FRANSI NYIMBO mwenye umri wa miaka 32 Mkazi wa mtaa wa mshikamo kata ya kipagamo katika halmashauri ya mji wa makambako amepewa adhabu ya kubeba mwili wa marehemu  CHRISTINA NYIMBO ambaye ni mwanae mwenye miezi tisa toka nyumbani hadi eneo la mazishi kwa kosa la kutoshiriki  shughuli za kijamii.

Akizungumza  mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mshikamano CHARLESI KIWALE amethibitisha kutolewa kwa adhabu hiyo ambapo ameeleza kuwa ndugu FRANSI NYIMBO amekuwa na kawaida ya kutoshirika shughuliza kijamii hususani kwenye matataizo  ya misiba huku ikielezwa kuwa ameshawahi kumtelekeza mke wake mpaka mauti yanamkuta hakuweza kushiriki kwenye mazishi hayo.


Aidha PHILIMONI NYIMBO ambaye ni kaka wa FRANSI NYIMBO ameeleza kuwa mdogo wake amekuwa na tabia ya kutoshiriki kwenye shughuli za kijamii na kutelekeza watoto hali ambayo inamfanya ashindwe kuelewa mdogo wake ameipata wapi hiyo tabia kwa kuwa ukoo wao wamekuwa hawana tabia kama hiyo.

Naye BRYSON NGONDE Ambye ni shemjeni wa FRANSI NYIMBO ameeleza kuwa tatizo la shemeji yake limeanza tangu mwaka jana mwenzi wa kumi na mbili baada ya dadake kuaza kuumwa ambapo alitelekezwa mpka mauti inamkuta hali ambayo imejirudia kwa sasa kutokana na leo kukamatwa na kulazimishwa kushiriki mazishi ya mwanae ambaye  enzi za uhai wake alimtelekeza kwa kutomhuumia kipindi anaumwa.

Hata hivyo kwa upande wake FRANSI NYIMBO amekana madai ya kumtelekeza mke wake pamoja na mwanae na kueleza kuwa chanzo cha hayo ambayo yametokea yamesababishwa na ndugu wa upande wa marehem mke Wake kwa kuwa wao ndio waliomchukua nyumbani kwake bila yaye kupewa taarifa,


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo