Polisi wa barabarani kisiwani pemba wakishirikiana na watendaji wengine kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’ wafanya zoezi la utambuzi wa bima halali, ambapo vyombo vya usafiri 71 walivigundua havina bima halali kati ya 168 walivyovihakiki.
POLISI wa usalama barabarani wakiwa kwenye zoezi maalum la kufanya uhakiki wa bima halali kw anjia ya mtandao, mara baada ya Polisi hao kupata mafunzo ya jinsi ya utambuzi wa bima zia kughushi, hivi karibuni kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MTOTO Fauzi Mohamed Subeit (16) mkaazi wa Mkoroshoni wilaya ya Chakechake, akizungumza na waandishi pamoja na Polisi wa usalama barabarani, baada ya kukamatwa akiendesha gari kinyume na sheria, wakati Polisi hao wakifanya uhakiki wa bima halali kw anjia ya mtandao, mara baada ya Polisi hao kupewa mafunzo na Mamlaka ya Usimamizi wa Bimta Tanzania TIRA, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
GAZRI kadhaa zikiwemo za kutembelea, za abiria, mzingo na vyombo vya magurudumu mawili zikiwa uwanja wa Gombani Chakechake, ili kufanyiwa ukiki wa namba za bima zao, na watendaji wa Polisi na wale kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MKUU wa kikosi cha uslama barabarani mkoa wa kusini Pemba Sahwali Abdalla Ali, akishiriki katika zoezi la utambuzi wa bima halali, akiwa na watendaji wengine kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’ ambapo vyombo vya usafiri 71 walivigundua havina bima halali katia 168 walivyovihakiki, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
BAADHI ya abiria walikuwa wakisafiri na gari mbali mbali za abiria, wakilazimika kutembea kwa miguu wakiwa na mizigo yao, baada ya gari walizokuwa wamepanda kufanyiwa uhakiki wa bima zao na kugundulika kuwa ni za kughushi, kwenye zoezi maalumu lililofanywa na Jeshi la Polisi na Mamlaka ya usimamizi wa bima Tanzania TIRA, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
DEREVA wa gari ya abiria ambae hakupatikana jina lake, akielezea mtazamo wake juu ya zoezi la uhakiki wa bima halali, lililofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, hivi karibuni kisiwani Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>> Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi