Wananchi
wilayani Makete mkoa wa njombe
wametakiwa kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa kwa kuwa
vitendo hivyo ni kinyume cha sheria.
Akizungumza katika
mkutano na viongozi wa chama cha
mapinduzi wa kata ya tandala katibu mkuu wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Lengae Godsoni Akyoo
amesema vitendo vya rushwa havina budi kukemewa kwa nguvu zote.
Bw.Akyoo ameongeza kuwa kuelekea katika uchaguzi wa ndani ya chama hicho vitendo vya rushwa hivitafumbiwa macho ili
kuweza kupata viongozi stahiki.
Alexanda Mbilinyi
ni mmoja ya wajumbe waliohudhuria katika
mkutano huo naye anakiri kuwepo kwa
vitendo vya rushwa katika jamii na hasa
nyakati za uchaguzi.
Katika hatua
nyingine mwenyekiti wa chama hicho
wilaya ya Makete BW. FRANSIS
CHAULA amesema ili kuimarisha demokrasia
mambo yote ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho yanatakiwa kufanyika kwa
uwazi.