Mwili wa Marehemu PRAISE ROLAND MWALYAMBI miongoni mwa watoto waliofariki juzi karatu Arusha kwa ajali ya gari, umezikwa saa 2 usiku katika makaburi ya Parokia ya Irambo, kijiji cha Irambo, kata ya ulenje Mbeya vijijini.
Mwili wa marehemu ulipokelewa na wana Mbeya saa 11 kasoro oil com nsalaga uyole ambapo mji wa uyole ulikumbwa na simanzi jioni ya jana kisha hasa kuanzia nsalaga hadi igawilo .
Kisha mwili kupelekwa hadi Irambo ukiongozwa na polisi chini ya mkuu wa wilaya ambapo tulifika Irambo nyumbani kwa Roland kisha kanisani kwa ajili ya Ibada ya kumuombea marehemu hadi saa 2 usiku alipozikwa kukiwa na giza na baridi haswa.
Imenibidi nihudhurie huu msiba maana Roland ni jirani kikata .
R.I.P Mwanawitu Praise




















