PICHA: Kiungo wa Yanga Justine Zulu ameshonwa nyuzi 9 baada ya kuumia

Kiungo wa kimataifa wa Yanga kutokea Zambia Justine Zulu leo April 1 2017 ameongezeka katika list ya wachezaji majeruhi wa Yanga ambao watakosekana uwanjani, Zulu ameongeza idadi ya majeruhi baada ya kuumia dakika ya 58 wakati wa mchezo dhidi ya Azam FC.
Zulu ambaye Tanzania kajizolea umaarufu kwa jina la mkata umeme alichezewa faulo na nahodha msaidizi wa Azam FC Himid Mao na kushindwa kuendelea na mchezo huo na kutolewa nje na nafasi yake ikachukuliwa na Emanuel Martin.
Taarifa za Zulu kutolewa na nje ya uwanja na kushonwa nyuzi 9 mguuni kwake kutokana na nyama zake za ugoko kuchimbika, anaungana kukaa nje ya uwanja na wachezaji wenzake Donald NgomaAmissi Tambwe na Thabani Kamusoko wanaouguza majeruhi, katika game hiyo Yanga ilipata ushindi wa goli 1-0.
Chanzo:millardayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo