Mauaji ya Polisi Kibiti yalivyomtesa Mtumishi wa Mungu

MHUBIRI wa Kanisa la IEACT lililoko Manispaa ya Shinyanga, Eliamani Kisanaga, amebubujikwa na machozi kutokana na vitendo vya kinyama vinavyoendelea hapa nchini vya kuuawa kwa polisi.

Kutokana na hali hiyo, aliwashauri Watanzania kumrudia Mungu kwa kuishi kwa kupendana kama alivyoagiza katika vitabu vitakatifu. Mhubiri huyo alitokwa na machozi wakati wa Misa ya Pasaka, iliyofanyika juzi, kwenye kanisa hilo. Pia alitumia fursa hiyo kuwaaga waumini wa kanisa hilo kuwa anahama. 

"Tuishi kama Kristu kwa kuiga matendo yake, tusijiite Wakristu tu bila matendo, huko ni kujidanganya kwani hakuna kitabu kinachohubiri kuua, hiyo ni njia ya shetani. Tunakokwenda Watanzania wenzagu ni kwenye laana," alisema. 

Aliongeza: "Nchi yetu katika sura ya kimataifa, tulikuwa na sura nzuri ya amani na upendo, lakini ghafla yakaanza mauaji ya vikongwe, mauaji ya walemavu wa ngozi, dawa za kulevya na leo tunaua askari wetu wanaotulinda, tunakwenda wapi?" 

Pia, aliwataka Wakristo kuishimaisha mema na kuwa mfano kwa watu wengine ambao si wakristo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo