Afariki Dunia kwa kutumbukia kisimani

Mtu mmoja ambae ni mgonjwa wa akili amefariki Dunia baada ya kutumbukia ndani ya kisima  kilichopo maeneo ya Sokoni mzuri Makunduchi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosibitiswa na kaimu kamanda wa Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Kheri Mussa kuwa marehe huyo aliyejulika kwa jina la Wanu Ameir Chum ambapo tukio hilo limetokea jana huko Mzuri Makunduchi.
Aidha Kamanda huyo alitoa wito wa watu wanaoishi na wagonjwa wa akili kuwa karibu nao na kutowaacha peke yao majumbani ili kuweza kuepusha majanga kama hayo.
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Koteji Makunduchi na kukabidhiwa kwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo