LHRC yataka RC Makonda achukuliwe Hatua

Na Maria Kaira
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimetoa wito kwa viongozi serikalini kuepuka kutumia vyombo vya dola katika kudidimiza uhuru wa vyombo vya habari kwa kuwa kitendo hicho kinavunja misingi iliyowekwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18.

Kituo hicho pia kimeitaka serikali kumchukulia hatua za kinidhamu na kijinai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa kitendo anachodaiwa kufanya Machi 18, 2017 cha kuvamia kituo cha Ofisi cha Clouds TV kufuatia kushindwa kushinikiza kurushwa kwa taarifa katika kipindi cha ‘The Weekend Chat Show’, kwa kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa kanuni za makosa ya adhabu  ya mwaka 2002.
.
Kauli hiyo ilitolewa Jana na mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho Dkt.  Helen Kijo Bisimba wakati akitoa tamko la kukemea uvamizi wa uhuru wa vyombo vya Habari alisema kituo cha kuvamia chombo cha Habari kwa kiongozi ni kigeni na cha kuogofya kwa watanzania.

“Viongozi kutotumia matumizi ya vyombo vya dola kwa manufaa binafsi, kama ilivyotumika kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds. Pia vyombo vya habari viungane kutetea masilahi ya uhuru wa habari na kuacha kujiendesha kwa masilahi binafsinhuku vikiacha weledi wa
vyombo hivyo ukizidi kudidimia,” amesema Kisimba.  

Ameongeza kuwa “LHRC tunaamini serikali kupitia viongozi wake wanafanya kazi kubwa katika kupambana na umasikini, kuboresha elimu, kupinga madawa ya kulevya  pamoja na rushwa, lakini tunazidi kusisitiza sana viongozi waheshimu misingi ya Utawala Bora na Haki za Binadamu ili kufikia haki na usawa. 

Alisema  kulingana na hali iliyoko sasa kituo hicho kitaendelea kukemea vitendo hivyo kwa kuwa vinadhalilisha serikali kitaifa na kimataifa kwa nchi inayojipambanua kuwa ni kisiwa cha Amani na mlinzi wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora wenye kulinda demokrasia.

"kwa Tukio la mkuu wa mkoa si la kiungwana haswa pale ambapo jambo hilo linafanywa na mtu mwenye mamlaka ya kuhakikisha utekelezwaji wa sheria na ulinzi wa amani katika Mkoa kwa mujibu wa sheria ya tawala za Mkoa kifungu cha 5 jambo hilo ni la kihuni na la kupingwa kinguvu katika Taifa linalofuata misingi ya haki na tawala za sheria "Bisimba

Alisema anasikitishwa kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya 5 ya kuhamasisha uwajibikaji na kutumia kauli ya hapa kazi tu kumuunga mkono mkuu huyo wa Mkoa ambaye amevunja sheria.. 

Alisema vyombo vya Habari vinapaswa kulindwa na kupewa ulinzi wa kutosha na si kuingiliwa mtu au mamlaka yeyote kwa manufaa binafsi yasoyo na tija kwa Taifa.

Alisema sheria ya huduma za vyombo vya Habari imeeleza wazi mamlaka ambazo zina weza kuviwajibisha vyombo hivyo pale vinapoonekana vinaendelea au vinatoa Habari za uchochezi na si kuvamiwa kwa siraha
"tumepokea kwa masikitiko makubwa kwa kile kinachodaiwa mkuu wa Mkoa kushirikiana kurushwa kipindi cha The weekend chat show kwakuwa kitendo hicho ni kukiuka misingi ya sheria "alisema Bisimba

Alisema vyombo vya Habari vinatakiwa kuungana kutetea maslahi ya uhuru wa Habari na kuacha kujiendesha kwa maslahi binafsi huku vikiacha weledi wa vyombo hivyo ukizidi kudidimia


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo