Kimeshanuka: Paul Makonda Apigwa Chini na Wanahabari

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) leo  limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Paul Makonda.

TEF wameyasema hayo leo katika  taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha.

“Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo