Uongozi wa serikali ya kijiji cha Korini kusini wilaya ya
Moshi Mkoani Kilimanjaro unamsaka mkazi wa kijiji hicho Deo Manga kwa tuhuma ya
ukatili dhidi ya mwanae Dorini Manga kwa kumvunja mkono wa Kushoto
Mtoto Dorini Ni mwanafunzi wa darasa la Kwanza katika
shule ya msingi Kiwalaa na alichapwa fimbo na baba yake mzazi hadi mkono
kuvunjika na kisha baba yake kutokomea
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi anakosoma mtoto huyo
Evance Tarimo amekiri kutokea kwa tukio hilo
Mtoto Dorini ameelezea sababu za kufanyiwa ukatili huo na
baba yake mzazi kuwa ni kuchelewa kutoka shuleni
Mwenyekiti wa kijiji hicho Emanuel Mrema ameahidi
mtuhumiwa huyo kukamatwa ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma
zinazomkabili