Waziri Mkuu akatisha ziara yake Mkoani Arusha

Waziri mkuu Mh Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuwachukulia hatua haraka watendaji wanaoendelea kuihujumu taasisi hiyo na kusababisha ikabiliwe na matatizo yanayotishia maisha ya wananchi ndani ya mamlaka hiyo, uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na watendaji wa mamlaka hiyo Mh Majaliwa pia  ameagiza kufanyika kwa sensa ya mifugo ili kijua idadi ya mifugo ya wenyeji na iliyoingizwa kutoka nje.

Pia waziri mkuu ameagiza kupatiwa taarifa ya mchanganua wa matumizi ya fedha zinazotolewa na mamlaka hiyo kwa ajili ya miradi ya wananchi na pia kuangalia uwezekano wa kuanza kuchimba visima vya maji kwa ajili ya wananchi na mifugo ili kuepusha mifugo kupelekwa kwenye maeneo muhimu ya utalii kwa kisingizio cha kufuata maji.

Akizungumza katika kikao hicho waziri wa maliasili na utalii Mh Prof Jumanne Maghembe pamoja na kuelezea hatua zinazochukuliwa kutatua matatizo ya Ngorongoro amemwomba waziri mkuu kuyafuta baadhi ya mashirika ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika wilaya hiyo ama kuyahamishia maeneo mengine kwani yana mchango wa matatizo yaliyopo.

Mhifadhi mkuu wa Ngorongoro Bw Fread Manongi, mbunge wa jimbo hilo Mh William Ole Nasha na mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo walimweleza waziri mkuu kuwa matatizo ni makubwa zaidi kuliko yaliyotajwa na njia pekee ya kuyatatua ni kuongeza ushirikishaji na usimamizi wa sheria.

Awali mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw Rashidi Mfaume Taka amesema kwa sasa umaskini, wa kipato kwa wananchi unaongezeka na baadhi ya maeneo yameanza kuwa na upungufu wa chakula.

Mh waziri mkuu amelazimika kukatisha ziara na amerejea jijini Dar es Salaam kutokana na kujitokeza kwa majukum mengine ya kikazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo