Afisa elimu shule za msingi wilaya ya Makete
Mwl.Antony Mpiluka ametolea ufafanuzi juu ya taarifa zilizokuwa zikienezwa kuwa
aliyekuwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Missiwa iliyopo katika kata ya
Ipelele wilayani Makete Bi.Gloria Simba ametoroka na kuitelekeza shule hiyo kwa
kuhofia kutumbuliwa kutokana na kughushi vyeti vyake vya kazi na kubainisha
kuwa mkuu huyo wa shule amehamishwa kwa taratibu kwenda shule ya msingi Ruaha
ambayo ni shule mpya.
Mwl.Mpiluka ametoa ufafanuzi huo leo alipokuwa
akizungumza na kituo cha redio Green Fm kwa njia ya simu katika mahojiano
maalum,ambapo amekanusha taarifa hizo huku pia akimtaja Furaha Fungo kuwa ndiye
atakuwa mbadala wa mkuu huyo wa shule.
Pia Mwl.Mpiluka ameelezea kusikitishwa kwake
kufuatia shule za msingi za kata ya Ipelele iliyopo katika tarafa ya Magoma
wilayani hapa kufanya vibaya katika matokeo ya darasa la saba mwaka huu kama
anavyoeleza.
Mwl.Mpiluka pia akaelezea hali halisi ya matokeo
ya darasa la saba mwaka huu huku akidai kuwa kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa
kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka jana.
Mwl.Mpiluka ametumia fursa hiyo pia kuzitaja shule
10 bora kwa wilaya ya Makete zilizofanya vizuri kwa matokeo ya darasa la saba mwaka
huu na shule 20 zilizofanya vibaya katika matokeo hayo.
Na Fadhili Lunati
Sikiliza sauti yake hapa chini:-