Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kumkamata mtu mmoja aitwaye NICODEMAS PIUS NGONYANI mkazi wa Peramiho Songea Mkoa wa Ruvuma akiwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilogram 61 na urefu wa sentimita 150 kila moja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari
Mtu huyo amekamatwa usiku wa kuamkia leo wakati jeshi la hilo kwa kushirikiana na Askari wa Wanyama pori TANAPA wakifanya msako wa pamoja katika maeneo ya shule ya msingi Sangambi, Kata ya Sangambi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya na
Aidha katika msako huo watuhumiwa wengine wawili wanaofahamika kwa sura walikimbia na kutelekeza pikipiki mbili zenye namba za usajili MC 466 ASU na T.285 CHP zote aina ya shaneray rangi nyekundu walizokuwa wamebebea nyara hizo. upelelezi unaendelea pamoja na msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliokimbia.