Rais Magufuli amjulia hali Mkuu wa Mkoa aliyelazwa Hospitali ya Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli, jana tarehe 19 Novemba, 2016 amemtembelea na kumjulia hali Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martin Shigella ambaye amelazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Bw. Martin Shigella alifikishwa hospitalini hapo tangu Jumatano iliyopita kwa ajili ya kupata matibabu.

Akimpa pole wodini humo Rais Magufuli alisema “Nakupa pole sana Ndg. Martin Shigella kwa maradhi yaliyokupata, nakuombea kwa Mwenyezi Mungu upone haraka na urejee katika kituo chako cha kazi ili uendelee na majukumu ya ujenzi wa Taifa”

Hali ya Bw. Martin Shigella inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo